Video pendwa ya wimbo wa nyota wa Bongo Flava na msanii wa Konde Music, Killy uliopewa jina la ‘Ni Wewe’ akimshirikisha staa wa muziki wa bongo na Boss wake, Harmonize imefutwa kwenye mtandao wa YouTube.
RELATED: Killy Ft Harmonize – Ni wewe (Prod. Hunter)
Video hiyo iliyoachiwa tarehe 13 Januari na ndani siku chache iliweza kufikisha zaidi ya watazamaji Millioni 1.5, iliondolewa YouTube baada ya kushtakiwa kwa tuhuma za hatimiliki na mtu anayefahamika kama Ian Mutisya Munyithya kutoka Kenya.
Ngoma hiyo tayari ilikuwa ishatazamwa zaidi ya mara milioni moja na ilikuwa imeshikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya ngoma zinazovuma zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania.
Akizungumza katika mahojiano na Rick Media, meneja wa Killy alisema kuwa timu ya Konde Music Worldwide inafuatilia suala hilo ili kuhakikisha kuwa video hiyo inarudishwa mtandaoni.
“Ni changamoto ambayo imetokea kweli, na hata sisi wenyewe imetupa hofu kujua ni nini tatizo linaloendelea huku mitandaoni. Kwa sababu mashabiki walikuwa wakisubiri sana video ya Ni Wewe ya Killy na ni wimbo ambao unafanya vizuri saa hizi. Na uko namba moja on Trending on YouTube.
RELATED: Killy – Mwisho (Prod. Neksazy)
Ni suala ambalo bado linafuatiliwa, kuna mtu ambaye anahusika na social media pale ofisini bado analifuatilia kujua tatizo ni nini,” meneja wa Killy alisema.
Video ya Killy na Harmonize yafutwa YouTube
Also, check more tracks from Harmonize;