C - NEWS

Marioo Adai Kuwekewa Sumu na Chino Kidd

Marioo Adai Kuwekewa Sumu na Chino Kidd

Kumekuwa na hali ya kutatanisha kati ya wasanii wawili maarufu wa Bongo Fleva, Marioo na Chino Kidd, ambao hapo awali walikuwa marafiki wakubwa. Hali hii imezuka baada ya Marioo kuamua kuvunja ukimya na kumuuliza Chino ni wapi alikosea, akidai kuwa amekuwa akimuunga mkono muda wote bila kujua ni kwanini sasa wanakuwa na tofauti.

RELATED: Alikiba – Top Notch Ft. Marioo

Kupitia ukurasa wake wa Insta-Story, Marioo ametoa dukuduku lake, ambalo kwa muda mrefu alikuwa amelinyamazia. Marioo ameeleza kuwa hajui ni nini alichomkosea Chino zaidi ya kumsaidia na kumpa sapoti katika safari yake ya muziki.

Marioo aliandika:
“Ndugu zangu, naomba mnisaidie kumuuliza Chino ni nini niliwahi kumkosea ambacho mimi sikijui, zaidi ya kumuonyesha sapoti? Ni nani kamwambia Chino kwamba ili aendelee kimuziki, ni lazima anidharaulishe na kuonekana ana matatizo na mimi?”

Kwa masikitiko zaidi, Marioo aliendelea kueleza kuwa chuki kati yao imekuwa kubwa kiasi cha kuamini kuwa huenda Chino alihusika katika tukio la kutuma watu wenye nia mbaya kumuwekea sumu siku chache zilizopita.

“Hii chuki imekuwa kubwa sana mpaka naanza kuamini pengine ni kweli alihusika kutuma watu waniwekee sumu. Namshukuru Mungu tulifanikiwa kuiwahi kabla haijanidhuru,” aliongeza Marioo, akitoa shutuma nzito dhidi ya Chino.

Marioo pia alifichua kuwa alikaa kimya mara ya kwanza Chino alipozungumza vibaya kumhusu kwenye mitandao ya kijamii, lakini baadaye Chino alikuja kumuomba msamaha na Marioo akamsamehe. Hata hivyo, Marioo sasa anashangazwa kuona Chino ameanza tena kumsema vibaya hadharani.

Marioo Adai Kuwekewa Sumu na Chino Kidd

“Naombeni mnisaidie kumuuliza, labda ana sababu za msingi zinazomsukuma kutaka kunilipizia ubaya licha ya mazuri yote niliyowahi kumfanyia hapo nyuma. Sasa nimeruhusu! Mumuulize kwa mic na kamera zote, nataka ajibu,” Marioo aliandika kwa uchungu.

Shutuma hizi zimevuta hisia na maswali mengi kutoka kwa mashabiki wa muziki, ambao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mzozo huu kati ya marafiki wa zamani. Je, ni kweli Chino alihusika katika tuhuma hizi nzito? Au kuna jambo la siri linaloendelea kati ya hawa wasanii? Ni wazi kuwa sintofahamu hii bado inaendelea, na mashabiki wanatarajia maelezo zaidi kutoka kwa pande zote mbili.

RELATED: Baddest 47 Ft. Chino Kidd – Humu Tu

Kwa sasa, Marioo amewaacha mashabiki wake wakiwa na maswali mengi na kusubiri majibu kutoka kwa Chino Kidd kuhusu hali halisi ya mgogoro huu.

Also, check more tracks from Marioo;

Leave a Comment