Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, ametangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga utakaofanyika Oktoba 19, 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11 jioni. Akiwa kwenye uzinduzi wa Tawi la Simba Mongolandege Ukonga, Dar es Salaam, Ahmed Ally alieleza umuhimu wa mashabiki kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho.
RELATED: Jux Ft. Diamond Platnumz – Ololufe Mi (Prod. S2kizzy)
Viingilio Vya Mechi ya Simba vs Yanga 19 Oktoba 2024 (Tickets)
Mechi ya Kariakoo Derby kati ya Simba SC na Yanga SC, moja ya michezo inayosubiriwa kwa hamu kubwa, itafanyika Jumamosi, Oktoba 19, 2024. Mchezo huu wa Ligi Kuu ya NBC utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Simba SC, wakiwa wenyeji, wametangaza viingilio vya mechi hii, vinavyolenga kutoa fursa kwa mashabiki wote kushiriki.
Ahmed Ally amesisitiza kwamba mashabiki wa Simba wanatakiwa kuhakikisha wananunua tiketi zao mapema kutokana na wingi wa mashabiki wanaotarajiwa kuhudhuria.
Hivi hapa viingilio vilivyotangazwa:
- VIP A: TZS 50,000
- VIP B: TZS 30,000
- VIP C: TZS 20,000
- Orange: TZS 10,000
- Mzunguko: TZS 5,000
Tiketi tayari zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao na vituoni kote jijini Dar es Salaam. Ahmed amewahimiza mashabiki wa Simba kununua tiketi zao mapema kwa sababu mchezo huu unatarajiwa kuvutia mashabiki wengi na tiketi zinaweza kuisha haraka.
Vituo vya Kununua Tiketi
- Lampard Electronics – Simba HQ, Msimbazi
- Vunja Bei Shops – Maduka yote (Dar es Salaam)
- New Tech General Traders – Yenu Bar
- Sabana Business Center – Mbagala Maji Matitu
- TTCL Shops – Dar es Salaam
- Juma Burrah – Msimbazi Center
- Halphani Hingaa – Oilcom Ubungo
- Mtemba Service Company – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo Rombo
- Mkaluka Traders Ltd – Machinga Complex
- Khalfani Mohammed – Ilala Bungoni
- Karoshy Pamba Collection – Dar Live
- Gisela Shirima – Dahomey Street
- Gwambina Lounge – Temeke Opp Duce
- Antonio Service Co. – Sinza na Kivukoni
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sovereign Co. – Kinondoni Makaburini
Njia Mbadala za Kununua Tiketi
Kwa wale wasioweza kufika vituoni, tiketi zinapatikana pia kupitia mitandao ya simu, njia inayowarahisishia mashabiki walioko mbali na vituo vya tiketi. Ahmed Ally amewashauri mashabiki kuwasili mapema uwanjani ili kuepuka msongamano na kuhakikisha wanaingia kwa utaratibu mzuri. Milango ya uwanja itafunguliwa mapema ili kuwapa nafasi mashabiki kufurahia burudani kabla ya mechi kuanza saa 11:00 jioni.
Tunahimiza mashabiki wote wa Simba kuungana kwa nguvu kushuhudia mchezo huu wa kihistoria!
Also, check more tracks from Alikiba;