C - NEWS

Mtangazaji Mahiri Khadija Shaibu ‘Dida’ Afariki Dunia 4 Oktoba 2024

Mtangazaji Mahiri Khadija Shaibu 'Dida' Afariki Dunia 4 Oktoba 2024

Tanzania imepoteza mmoja wa watangazaji wake mahiri, Khadija Shaibu maarufu kama Dida, ambaye amefariki dunia jioni ya leo, Oktoba 4, 2024. Taarifa za msiba huu zimethibitishwa na mtangazaji mwenzake na rafiki wa karibu, Maulid Kitenge, kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii. Kitenge aliandika, “Dida Shaibu wa Wasafi FM Amefariki dunia.”

RELATED: Whozu Ft Zuchu – Attention (Prod. S2kizzy)

Uongozi wa Wasafi Media umetoa taarifa rasmi ya huzuni, ukieleza kuwa Dida, aliyekuwa mtangazaji wa kipindi maarufu Mashamsham cha Wasafi FM, ameacha na pengo kubwa katika tasnia ya habari. Alijulikana kwa uhodari wake wa hali ya juu, ubunifu na uwezo wa kipekee ambao ulimfanya kuwa mtangazaji wa kike namba moja nchini. Alikuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake na watangazaji wengi waliokuwa wakimchukulia kama kioo cha mafanikio.

Tunashirikiana na familia, marafiki, na wadau wa tasnia ya habari katika kuenzi maisha ya Dida na mchango wake mkubwa kwa jamii na vyombo vya habari. Mola ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

Also, check more tracks from Zuchu;

Leave a Comment