C - NEWS

Diamond Platnumz Ajipanga kuachia Wimbo Mpya ‘Holiday’

Diamond Platnumz Ajipanga kuachia Wimbo Mpya 'Holiday'

Mfalme wa Muziki, SIMBA 🦁 Diamond Platnumz, anaendelea kuthibitisha umahiri wake kwa kutoa muziki wa kiwango cha juu ndani ya muda mfupi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameweka kionjo cha wimbo wake mpya kwa kushiriki video fupi akiwa kwenye gari pamoja na mtayarishaji maarufu ZOMBIE, S2kizzy.

RELATED: Diamond Platnumz – Mapoz Ft Mr. Blue & Jay Melody

Wiki chache zilizopita, ‘Diamond’ alidokeza kuachia hitsong mpya, ikiwa ni miezi miwili tu tangu aachie wimbo wake maarufu ‘Komasava‘, ambao umefanikiwa kwa kiasi kikubwa duniani na hata kufikia chati za ‘Billboard Marekani (Billboard US Afrobeats)’.

Sasa, Diamond ameweka kionjo cha ngoma yake mpya aliyoiita ‘Holiday‘, ambayo inakuja rasmi wakati huu wa msimu wa joto (Summer), ambapo wengi duniani huchukua mapumziko na kufurahia likizo zao. Mashabiki wake wanapaswa kujiandaa kupokea kwa hamu wimbo huu mpya wa ‘Holiday’ ambao unaweza kuachiwa wakati wowote.

Hii yote inakuja baada ya nyota mwenzake, Ali Saleh Kiba, anayejulikana kama Ali Kiba au King Kiba, kuachia EP yake mpya iitwayo Starter. Hivyo basi, mashabiki wa muziki wa Bongo Flava wanatarajia burudani kali kutoka kwa wakali hawa wawili!

Also, check more tracks from Diamond Platnumz;

Leave a Comment