Alikiba, mwanamuziki maarufu wa Tanzania na mmiliki wa Kings Music na Crown Media Group, ameamua kuondoa mmoja wa watangazaji maarufu wa Clouds FM, Mwijaku, na kumsajili kwa Crown Media.
RELATED: Alikiba – Ndombolo Ft Abdukiba x K2ga x Tommy Flavour (Prod. Yogo)
Ijumaa hii, Alikiba alitangaza kupitia Instagram kwa kupost video fupi ikionyesha Mwijaku akiwa amepotea na baadaye kuokolewa na Alikiba. Aliandika: “Haloooo! Miongoni mwa watu niliowafikiria kuanzisha CROWN Media ni pamoja na wewe @mwijaku. Karibu sana Nyumbani 92.1 tuwapashe habari Watanzania.”
Karibu @crownfmtz @crowntvtz
HapaNiNyumbani #KingKiba