Habari ya kusikitisha imetufikia kuhusu kifo cha Noel Mwingila, maarufu kama Zuchy, ambaye alikuwa mpiga picha na mwandishi wa habari wa @millardayo na @ayotv_. Zuchy alifariki dunia mapema Alfajiri ya leo baada ya kupata ajali ya pikipiki eneo la Makonde – Mbezi, jijini Dar es Salaam. Chanzo cha karibu kimeithibitisha habari hii.
RELATED; Amos & Josh Ft King Kaka – Baadaye
Zuchy anatambulika kama mmoja wa wapiga picha mahiri katika tasnia ya habari na matukio. Wasafi Media tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, na timu nzima ya Millard Ayo & Ayo TV kwa msiba huu mzito. Tunamuombea Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.