Mfalme Mzee Yussuf ameshare picha akiwa na Diamond Platnumz kwenye Ukurasa wake wa Instagram, ambayo imewaacha mashabiki wengi na maswali .
Mzee Yussuf hivi Karibuni ameacha fumbo kubwa lisilokua na majibu, kutokana na kauli yake inayosema anataka Kurudi Mjini.
RELATED: Diamond Platnumz – Jeje
Wengi wameitafsiri kauli hiyo kwa namna tofauti, lakini kitendo cha kupost picha akiwa na SIMBA, kimezidi kuibua mijadala upya.
Kupitia ukurasa wake Mzee Yussuf alipost picha hiyo nakuandika:-
” Wakati umewadia kurudi town nadhani sasa mmeelewa tatizo si ndio maneno sasa yatakwisha, haya wale wenye aya mifukoni mwao nwale walokariri ukharamu na uhalali wafunge midomomo yao waniache nirudi mjini #NARUDIMJINI #SAFINA liko tayari kuondoka ahsanteni kwa kuja #FULLDOZ is coming nend kafanye ku subscribe chanel yangu Mzee Yusuph” .- Mzee Yussuf
Je , unadhani kuna Jambo gani kati ya mzee Yussuf na SIMBA!?