Januari 14, 2024 – Ni siku ya majonzi kwa familia ya Gerald Hando, mtangazaji maarufu wa Wasafi FM, kwani amepoteza mke wake mpendwa, Bi. Mariam Hando. Msiba huu umegusa mioyo ya wengi, na msiba utakuwa nyumbani kwao Mbezi Beach, Dar es Salaam.
- RELATED: Diamond Platnumz Ft Khadija Kopa – Nasema Nawe
- RELATED: Rayvanny Ft Diamond Platnumz – Vumbi (Prod. S2kizzy)
- RELATED: Diamond Platnumz – Jeje (Prod. Kel P)
- RELATED: Zuchu Ft Mbosso – Ashua
Kwa niaba ya familia ya Wasafi Media, tunatoa pole zetu za dhati kwa Gerald Hando, familia yake, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Tunaungana kwa pamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kuomboleza. Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki cha majaribu na huzuni.
Marehemu Mariam Hando atapumzishwa katika makaburi ya Kisutu. Taratibu za mazishi zinaanza leo, ambapo mwili wa marehemu utachukuliwa kutoka Hospitali ya Muhimbili saa 5:00 asubuhi. Tunawaomba wote wanaoweza kushiriki katika shughuli za mazishi, kufika na kuwa sehemu ya kuipa heshima ya mwisho roho ya marehemu.
Tunaiombea roho ya Mariam Hando, Mungu ailaze mahali pema peponi. Amen.
Poleni sana kwa msiba huu mzito. #WasafiMedia #PoleniFamiliaYaHando