ENTERTAINMENT

Fanya Tendo la Ndoa mara Tatu au Nne kwa Wiki Usipate UTI

Fanya Tendo la Ndoa mara Tatu au Nne kwa Wiki Usipate UTI

Tendo la ndoa ni sehemu muhimu ya maisha ya wanandoa, lakini linaambatana na hatari zake, hasa linapofanyika mara kwa mara. Moja ya matatizo yanayoweza kujitokeza ni maambukizi ya njia ya mkojo (UTI). Kwa mujibu wa Dr. Ikrah Abdallah, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, tendo la ndoa linapoongezeka maradufu linaweza kuwa chanzo cha hatari hii.

Dr. Abdallah anaeleza kuwa, kwa wanawake, vijidudu vinavyotoka nje ya mwili na kuingia ndani kupitia njia ya mkojo wakati wa tendo la ndoa vinaweza kuongeza kasi ya maambukizi ya UTI

Hii ni kwa sababu njia ya mkojo ya mwanamke iko karibu na eneo la uke, hivyo kuifanya iwe rahisi kwa vijidudu kusafiri na kuingia ndani.

Ili kupunguza hatari ya kupata UTI, Dr. Abdallah anashauri kwamba tendo la ndoa lifanyike kwa kiasi – mara tatu au nne kwa wiki. Hii itapunguza mzunguko wa vijidudu kuingia kwenye njia ya mkojo mara kwa mara. Aidha, ni muhimu kuzingatia usafi na afya binafsi.

Jambo jingine muhimu la kuzingatia ni tabia ya kujisafisha mara baada ya kumaliza tendo la ndoa. Kukojoa au kutoa haja ndogo mara tu baada ya tendo la ndoa husaidia kusafisha njia ya mkojo na kutoa vijidudu vilivyoingia.

Hii ni njia asili ya mwili kujikinga na maambukizi, kwani mkojo husaidia kusukuma na kutoa bakteria walioweza kuingia katika njia ya mkojo.

Leave a Comment