Kila taifa lina sheria zake mbalimbali juu ya swala la utoaji mimba. Katika nchi nyingi zilizoendelea utoaji mimba sio jambo la kusangaza.
Lakini jamii za kimila au kidini hasa Africa utoaji mimba sio jambo linalokubalika katika ngazi ya jamii, kidini na hata kisheria.
Ukweli ni kwamba kuotoa mimba ni sawa na kuuwa. Ukweli ni kwamba kama wazazi wako wangetoa mimba yako basi usingekuwa hapo kutoa mimba uliyonayo.
Lakini katika sheria za nchi yetu (Kenya) kuna kesi za kiafya ambazo hupelekea watu kuruhusiwa kutoa mimba. Makala hii ni kwa ajili ya watu ambao wanashida za kiafya zinazopeleka kulazimika kutoa mimba.
RELATED: Siku za kupata au kushika mimba (Jifunze hapa)
Pia kwenye nchi ambazo utoaji mimba unaruhusiwa, madaktari wengi hupendekeza kutumia dawa za utoaji mimba mifepristone na misoprostol ndani ya wiki 10 za mwanzo za mimba, lakini misoprostol ina ufanisi mkubwa pia kama unajaribu kutoa mimba ndani ya wiki 10 za mwanzo.
Dalili zake ni sawa sawa na zile za mimba kuharibika, na dawa za utoaji mimba ni salama kwa wanawake kutumia faragha.
Dawa zinazotumika kutoa mimba zinafanya kazi kwa kulegeza na kufungua taratibu shingo ya mfuko wa kizazi (mlango wa kizazi), na kusababisha mfuko wa kizazi kukaza ambayo inasukuma mimba nje ya kizazi.
Kwa kutumia Misoprostol, kwa kawaida katika saa 1 au 2 baada ya vidonge vya kwanza kuingia mwilini mwako, utaanza kuumwa tumbo na damu kutoka.
Kwa kawaida mimba itatoka ndani ya masaa 24 baada ya kunywa vidonge vya mwisho vya misoprostol, mara nyingi mimba inatoka kabla ya muda huo.
Kama unafuatilia vizuri, unaweza kujua mabaki ya mimba yanavyotoka. Unaweza kuona vitu kama vile zabibu ndogo nyeusi kidogo na utando mwembamba, au kifuko kidogo kilichozungukwa na utando mlaini mweupe.
Kutegemeana na umri wa mimba, tishu hizi zinaweza kuwa ndogo kuliko ukucha wako hadi kufikia ukubwa wa kidole gumba. Kama unaweza kutambua mabaki haya, ni dalili kuwa utoaji mimba umefanikiwa.
RELATED: Ni mikao ipi (staili) ambayo ni mizuri zaidi kuitumia kufanya wakati wa ujauzito?
Mara nyingi mabaki ya mimba yanaweza kuwa ndani ya mabonge ya damu. Unaweza usione mabaki haya isipokuwa ukiwa makini sana.